Jaji mstaafu wa Mahakama ya rufaa Damian Lubuva ambae ni
mwenyekiti wa tume ya Taifa ya Uchaguzi amesema tume ya uchaguzi imeahirisha uchaguzi kwa kata nne za Arusha kutokana na uwezekano wa wapiga kura kutoshiriki vyema katika zoezi la kupiga kura baada ya bomu kujeruhi na kuua jana.
“Tume imeahirisha uchaguzi katika kata nne za Arusha mjini
kutokana na tukio hilo ambalo linawapa Wananchi hofu wakati wa kupiga
kura hivyo uchaguzi umeahirishwa hadi tarehe 30 June”
Alifafanua zaidi kuwa “Jioni ya June 15 2013
tulipata taarifa ya tukio kule Arusha ambako uchaguzi unafanyika katika
kata nne za pale mjini, katika kata moja wapo ya kumalizia kampeni za
mwisho bomu likatupwa na watu kufariki pamoja na wengine kuumia,
kutokana na hilo tumeona sio wakati muafaka kwa uchaguzi kuendelea kwa
sababu wengine wanaendelea na shughuli za mazishi” alisema Lubuva.go
0 comments:
Post a Comment