MWANAMKE
mmoja anayefahamika kwa jina la Taraji Muenzi, 31, mkazi wa kijiji cha
Mwatasi, wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, anashikiliwa na jeshi la
Polisi mkoani humo kwa kosa la kuichoma nyumba ya jirani yake na
kuwateketeza watoto wawili waliokuwa ndani mwake pamoja na vitu vyote
katika nyumba hiyo kwa kilichoelezwa wivu wa mapenzi.
Habari kutoka mkoani humo zinasema watoto walioteketezwa wakiwa ndani ya nyuma hiyo ni Faraji, 6 na Jacob, 3 ambao walikuwa watoto pekee wa Subira Kisitu aliyekuwa akituhumiwa na mtuhumiwa huyo kuwa anatembea na mumewe.
Inaelezwa kuwa Taraji kwa muda mrefu alikuwa akimtuhumu jirani yake kumuibia mume na kumtishia kwamba atamfanyizia, kiasi cha uongozi wa eneo lao kuitisha kikao na kumtoza faini ya Sh 10,000 aliyotakiwa kuilipa juzi, Juni 22 siku aliyofanya tukio hilo.
Inaelezwa uongozi wa
kitongoji hicho kiliamua kumtoza faini baada ya wiki iliyopita kumvamia
jirani yake nyumbani kwake na kumwagia mboga na kusisitiza kuwa kuna
kitu atakachomfanyia ambacho hatasahau maishani kama siyo kwa kumuua kwa
sumu basi kwa kumchomea moto nyumba yake.
Hata hivyo inaelezwa kuwa jana juzi usiku akiamini kuwa jirani yake yupo ndani na wanawe aliamua kuichoma moto nyumba hiyo, ila kwa bahati mbaya jirani zake alikuwa klabuni akipata kinywaji na hivyo watoto pekee waliokuwa wamelala ndani ndiyo waliougua na kufa pamoja na mali zote.
Kamanda wa Polisi wa Iringa, Ramadhani Mungi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza wanamshikilia mwanamke huyo ili kumfikisha mahakamani kwa kitendo alichokifanya ambacho kimeacha gumzo kijiji cha Mwatasi, huku familia ya watoto ikiwa katika majonzi makubwa ya kupoteza watoto wao.
Via Mwakyjuniorblog
0 comments:
Post a Comment