Frank Lampard
Frank Lampard (Kushoto) na wenzake
Kiungo mkongwe wa Chelsea Frank Lampard ameiwezesha  timu yake kurejea katika nafasi ya tatu katika ligi kuu England baada ya kuifungia timu yake mabao mawili wakati vijana hao wa Stamford Bridge wakishinda magoli 2 – 1 dhidi ya Everton siku ya  Jumapili.

Everton ambao walikuwa nyumbani Goodson Park walipata goli lao mapema kabisa dakika ya pili ya mchezo  kupitia kwa kiungo wao toka Afrika Kusini.
Kwa ushindi huo Chelsea imefikisha pointi 38 katika nafasi ya tatu huku ikizidiwa na vinara Manchester United wenye pointi 49 na Manchester City iliyo katika nafasi ya pili kwa ponti 42.

Baadhi ya mashabiki wamekosoa uongozi timu hiyo kumuonesha mlango wa kutokea kiungo huyo mwenye miaka 34 kwa madai kuwa amechoka na atafute timu ya kuchezea wakati wa usajili wa dirisha dogo Januari 2013.
Tayari klabu ya Los Angels Galax ya Marekani imetoa ofa kwa kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza ili kuchukua nafasi ya mwingereza mwenzake David Beckham ambaye amemaliza mkataba wake na Galax.
Lampard atalipwa mshahara mnono  sawa na aliokuwa akilipwa  Beckham hivyo kumfanya mwanasoka anayelipwa zaidi katika ligi kuu Marekani.

 LUIS SUARES APIGA 2 LIVERPOOL IKISHINDA 3 – 0 DHIDI YA QPR.
Wachezaji wa Liverpool Wakishangilia Ushindi
Vijogoo wa Anifield Liverpool wameweza kuingia katika 10 BORA katika msimamo wa Ligi kuu nchini England baada ya kuitandika Queens Park Rangers(QPR) kwa magoli 3 – 0.
Mshambuliaji raia wa Uruguay Luis Suarez alifunga magoli mawili huku beki Daniel Agger akifunga bao la tatu kwa kichwa bomba baada ya kupata krosi kutoka kwa nahodha Steven Gerrard.

MSIMAMO LIGI KUU ENGLAND


Pos
Team
P
W
D
L
GF
GA
GD
Pts
1
Man Utd
20
16
1
3
50
28
22
49
2
Man City
20
12
6
2
38
19
19
42
3
Chelsea
19
11
5
3
39
18
21
38
4
Tottenham
20
11
3
6
36
26
10
36
5
Arsenal
19
9
6
4
39
21
18
33
6
Everton
20
8
9
3
33
25
8
33
7
West Brom
20
10
3
7
28
25
3
33
8
Stoke
20
6
11
3
21
17
4
29
9
Liverpool
20
7
7
6
31
26
5
28
10
Swansea
20
7
7
6
29
24
5
28
11
Norwich
20
6
7
7
23
32
-9
25
12
West Ham
19
6
5
8
22
23
-1
23
13
Sunderland
20
5
7
8
21
26
-5
22
14
Fulham
20
5
6
9
30
36
-6
21
15
Newcastle
20
5
5
10
26
37
-11
20
16
Wigan
20
5
3
12
22
35
-13
18
17
Aston Villa
20
4
6
10
15
39
-24
18
18
Southampton
19
4
5
10
26
37
-11
17
19
Reading
20
2
7
11
22
37
-15
13
20
QPR
20
1
7
12
16
36
-20
10
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top