Kufuatia tukio la mauaji lililotokea Mkoani Kagera katika kijiji cha Mgoma Tarafa ya Kanazi, Wilaya ya Ngara tarehe 15 mwezi Disemba, 2012 na kusababisha kifo cha Sande John na askari wawili namba E.579 CPL PASCAL na namba H.429 PC ALEXANDA.

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Saidi Mwema amepeleka Mkoani Kagera timu maalum ya uchunguzi kutoka Makao Makuu ya Polisi, inayohusisha Idara ya Upelelezi  na Kamisheni ya Oparesheni, ili kuungana na timu ya upelelezi ya Mkoa kuchunguza zaidi tukio hilo na kuwabaini wote
waliohusika katika kusababisha vifo kwa askari na raia pamoja na madhara mengine dhidi ya mali.

Wakati uchunguzi huo ukiendelea, Jeshi la Polisi linawaomba wananchi kuwa watulivu, hususani wananchi wa Mkoa wa Kagera na waendelee kutoa ushirikiano wa dhati kwa Jeshi la Polisi ili wahalifu hao wachache wanaotumia kisingizio cha hasira kali waweze kukamatwa na sheria
kuchukua mkondo wake.
Imetolewa na:-
Advera Senso-ASP
Msemaji wa Jeshi la Polisi(T)
Polisi Makao Makuu. TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top